Loading...

Mashabiki watakaoingia taifa leo kushuhudia mechi ya Simba na Yanga kupimwa kilevi

MASHABIKI wote watakaoingia Uwanja wa Taifa leo kushuhudia mtanange wa watani wa jadi Simba na Yanga, watalazimika kupimwa kama wametumia kilevi (pombe) kwa lengo la kudhibiti fujo ndani ya uwanja.

Hayo yamesemwa na Jeshi la Polisi nchini kupitia kamanda wa jeshi hilo Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro ambaye ameweka wazi kuwa kitakuwapo kifaa maalumu cha kupima kilevi milango yote ya kuingilia.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Kamanda Sirro, alisema jeshi hilo halitaruhusu mtu yeyote aliyetumia kilevi kuingia uwanjani lengo likiwa ni kuepusha vurugu zisizokuwa za lazima.

Alisema pia kutakuwa na askari polisi waliovaa kiraia wakiwa na kamera na vinasa sauti ili kubaini mbinu zozote za uvunjifu wa amani na kwamba, atakayenaswa akijaribu kuleta fujo cha moto atakiona.

“Hairuhusiwi kuingia na maji wala silaha uwanjani kwa kuwa wengi huweka viroba katika chupa na kudai maji, maji yatauzwa ndani.

“Mechi iliyopita jeshi hili lilidhalilishwa sana kwa mashabiki kung’oa viti mbele ya vyombo vya dola, lakini katika mechi ya kesho (leo) sitakubali na nina usongo na watakaothubutu kufanya vurugu,” alisema Sirro.

Alisema wamefunga kamera za CCTV nyingi nje na ndani ya uwanja zitakazowabaini watakaoanzisha vurugu na uhalifu uwanjani hapo, ambapo amewatahadharisha wenye tabia za kuanzisha vurugu kutothubutu kufanya hivyo kwani wataumbuka.

Source: Bingwa
Mashabiki watakaoingia taifa leo kushuhudia mechi ya Simba na Yanga kupimwa kilevi Mashabiki watakaoingia taifa leo kushuhudia mechi ya Simba na Yanga kupimwa kilevi Reviewed by Zero Degree on 2/25/2017 11:52:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.