Haya hapa Matokeo ya Darasa la 7

Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba uliofanyika kuanzia Septemba 10, 2025.
Matokeo hayo yametangazwa leo, Jumatano Novernba 5, 2023 na Katibu Mtendajï wa Necta, Profesa Said Ally Mohamed.
Jumla ya watahiniwa 1,17 2, 279 walifanya mtihani huo kati ya hao wavulana ni 535,138 sawa na asilimia 45.65 na wasichana ni 637,141 sawa na asilimia 54.35.
Ufaulu wa jumla wa mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2025 umeongezeka kwa asilimia 0.93, ambapo jumla ya watahiniwa 937,581 sawa na asilimia 81.80 kati ya 1,146,164 waliofanya mtihani huo wamefaulu kwa kupata madaraja ya A, B na C.
Takwimu hizo zimetolewa leo na Necta, zikionesha ongezeko la ufaulu ukilinganisha na mwaka 2024 ambapo watahiniwa waliofaulu walikuwa asilimia 80.87.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kati ya waliofaulu, wavulana ni 429,104 sawa na asilimia 82.51, huku wasichana wakiwa 508,477 sawa na asilimia 81.21.
Aidha, Necta imeeleza kuwa ubora wa ufaulu nao umeimarika, ambapo jumla ya watahiniwa 422,923 sawa na asilimia 36.90 wamepata madaraja ya juu (A na B), kilinganishwa na asiliia 35.83 mwaka 2024 sawa na ongezeko la asilimia 1.07.
Haya hapa Matokeo ya Darasa la 7
Reviewed by Zero Degree
on
11/05/2025 02:50:00 PM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
11/05/2025 02:50:00 PM
Rating: