Loading...

Kiongozi wa ulanguzi wa dawa za kulevya akamatwa nchini Tanzania

Maafisa wa polisi nchini Tanzania wanasema kuwa wamemkamata kiongozi wa ulanguzi wa dawa ya kulevya aina ya heroine anayefanya operesheni zake kati ya Afrika mashariki na China.

Maafisa hao wanaokabiliana na ulanguzi wa mihadarati wanasema kuwa Ayub Mfaume ambaye anajulikana kama kiboko alikuwa mmoja wa watu wanaotafutwa sana nchini humo.

Anadaiwa kuwa na ushiirikiano na walanguzi wa mihadarati nchini Brazil, Pakistan, na mataifa kadhaa ya Ulaya.

Maafisa hao wanasema kuwa Bwana Mfaume alijisalimisha kwa maafisa hao kufuatia msako wa wiki mbili dhidi ya walanguzi wa mihadarati.
Kiongozi wa ulanguzi wa dawa za kulevya akamatwa nchini Tanzania Kiongozi wa ulanguzi wa dawa za kulevya akamatwa nchini Tanzania Reviewed by Zero Degree on 2/25/2017 11:08:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.