Loading...

Kiungo wa Zesco ya Zambia kutua Msimbazi?

BAADA ya Yanga kushindwa kumsajili Mzambia, Mishack Chaila, Simba wameingia miguu yote kwa injini hiyo kimya kimya kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Chaila ambaye aliwahi kufundishwa na kocha wa sasa wa Yanga, George Lwandamina, katika kikosi cha Zesco United ya Zambia, awali alikuwa akitajwa kusajiliwa na Wanajangwani hao katika dirisha dogo la usajili lakini ikashindikana.

Yanga walimhitaji kiungo huyo mwenye umbo refu, nguvu na uwezo wa kutumia miguu yote akiwa tegemeo katika kikosi cha timu ya Taifa ya Zambia.

Chaila ana uwezo wa kucheza vyema kama kiungo mkabaji kama anavyotumiwa na kocha wa timu hiyo lakini pia ana uwezo wa kucheza kama kiungo mshambuliaji na pembeni.

Kiungo alisema kwamba, anatamani kucheza nchini (Tanzania) katika timu yoyote itakayomhitaji kwani amesikia kuna masilahi manono.

Alisema baada ya kushindwa kujiunga na Yanga msimu huu kutokana na mkataba wake kumbana, ana imani msimu ujao utakuwa rahisi kwake kutokana na mkataba wake kumalizika.

“Nadhani hakuna mchezaji asiyependa kutoka nje na nchi kwenda kucheza soka, kikubwa ni masilahi, natamani sana kucheza soka nchi ambayo anafundisha kocha wangu,” alisema.

Chaila alisema kama atakosa nafasi ya kuchezea timu anayofundisha Lwandamina kwa muda huu, basi ana imani kubwa atajiunga na mahasimu wao Simba kama watahitaji huduma yake.

Source: Dimba
Kiungo wa Zesco ya Zambia kutua Msimbazi? Kiungo wa Zesco ya Zambia kutua Msimbazi? Reviewed by Zero Degree on 2/05/2017 04:48:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.