Loading...

Makamanda wa jeshi wajiuzulu Sudan Kusini

Rais Salva Kiir
Maafisa watatu wakuu wa kijeshi ndani ya serikali ya Sudan Kusini, wamejiuzulu.

Makamanda hao wamejiondoa serikalini wakimlaumu Rais Salva Kiir kwa kuhusika katika uhalifu wa kivita na mauwaji yanayolenga kabila fulani.

Brigedia Henry Oyay Nyago, anamshutumu Rais, ambaye anatoka katika kabila la Dinka, kwa kuamuru kuawawa kwa watu wasiotoka katika kabila hilo la Dinka.

Kanali Khalid Ono Loki, pia anamlaumu kiongozi mkuu wa jeshi kwa mauwaji ya kimbari, kukamatwa na kuwazuilia watu kiholela.

Source: BBC Swahili
Makamanda wa jeshi wajiuzulu Sudan Kusini Makamanda wa jeshi wajiuzulu Sudan Kusini Reviewed by Zero Degree on 2/19/2017 12:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.