Loading...

Serikali yawasafirisha watanzania waliofukuzwa Msumbiji

Baada ya Watanzania wanaoishi nchini Msumbiji kufanyiwa vitendo vya kikatili na kufukuzwa, Serikali mkoani hapa imelazimika kuwasafirisha kwa kutumia magari ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ili kuwafikisha karibu na mikoa wanakotokea.

Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara, Rose Mhagama amesema hadi kufikia juzi, Watanzania waliojisajili katika mpaka wa Kilambo wakitokea Msumbiji walikuwa 220.

Amesema tayari watu 109 wa awamu ya kwanza wamesafirishwa, ambao waliishukuru Serikali na wakazi wa Mtwara kwa kuwapokea na kuwapa misaada mbalimbali.

Mmoja wa waliorudishwa, Mwajuma Abdallah amesema: “Tunawashukuru wanamtwara na Serikali kwa jumla kwa kutupokea vizuri leo (jana) tunarudi nyumbani.”

Source: Mwananchi
Serikali yawasafirisha watanzania waliofukuzwa Msumbiji Serikali yawasafirisha watanzania waliofukuzwa Msumbiji Reviewed by Zero Degree on 2/19/2017 10:56:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.