Loading...

Mashamba ya bangi yenye zaidi ya ekari mia moja na ishirini yakamatwa wilayani Tarime.

Vyombo vya dola katika kanda maalum ya Tarime na Rorya mkoani Mara kwa kushirikiana na watendaji mbalimbali wa serikali wilayani Tarime,vimendelea na oparesheni kali ya kupambana na kilimo cha zao haramu la bangi na kufanikiwa kukamata mashamba yenye ukubwa wa zaidi ya ekali 120 ambayo yamelimwa katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo kisha kufyekwa na kuteketezwa kwa moto.

Oparesheni hiyo kali na ya aina yake kwa mara nyingine imefanyika katika wilaya ya Tarime,ikiongozwa na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama,ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Tarime Bw Glorious Luoga,zoezi ambalo limetajwa kuwa na mafanikiwa makubwa katika kupambana na kilimo hicho cha zao hilo haramu la bangi wilayani Tarime.

Naye afisa tarafa wa Inano wilayani Tarime Bw Chacha Marwa,amesema kuwa wamebaini kuwa kila kaya ambayo inaishi katika kitongoji cha Kelenge wilayani Tarime,inamiliki shamba la bangi lenye ukubwa wa nusu ekali hadi ekari moja,ambayo imepandwa kuzunguka katika moja ya mto ndani ya kitongoji hicho.

Kwa upande wao baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani Tarime,wameonesha kusikitishwa na tabia ya baadhi ya wananchi wa wilaya ya tarime, kutumiwa na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa kutoka nchi jirani kulima zao hilo haramu,huku wakishindwa kutumia ardhi hiyo kulima mazao mengine ya chakula na biashara.

Source: ITV
Mashamba ya bangi yenye zaidi ya ekari mia moja na ishirini yakamatwa wilayani Tarime. Mashamba ya bangi yenye zaidi ya ekari mia moja na ishirini yakamatwa wilayani Tarime. Reviewed by Zero Degree on 2/24/2017 06:49:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.