Loading...

Rais Magufuli amefanya uteuzi mwingine

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 24 Februari, 2017 amemteua Dkt. John Kedi Mduma kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. John Kedi Mduma umeanza tarehe 23 Februari, 2017.

Dkt. John Kedi Mduma ni Mhadhiri Mwandamizi, Idara ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Dkt. John Kedi Mduma anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bi. Grace Rubambey ambaye amemaliza muda wake.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Rais Magufuli amefanya uteuzi mwingine Rais Magufuli amefanya uteuzi mwingine Reviewed by Zero Degree on 2/24/2017 06:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.