Loading...

Mwanariadha afa baada ya kuanguka ghafla kwenye mashindano ya Kili Marathon

MWANARIADHA wa Kenya, Charles Malowa (36) amekufa baada ya kuanguka kwenye mashindano ya Kili Marathon mkoani Kilimanjaro jana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alithibitisha kutokea kwa kifo hicho, akisema mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya KCMC.

Habari zinasema mwanariadha huyo alianguka ghafla akiwa anakimbia na wenzake katika mbio hizo.

Mratibu wa mashindano hayo, John Bayo aliliambia gazeti hili kuwa alifuatwa na wanariadha kutoka Kenya wakimjulisha mwenzao alianguka na walipomfikisha hospitali alikuwa ameshafariki.

Alisema Wakenya hao walimkabidhi namba ya mwenzao na kuomba wapatiwe medali ya ushiriki, fulana na namba kwa ajili ya kumbukumbu ya mwenzao, jambo ambalo alilitekeleza.

Katibu Mkuu wa Riadha Tanzania (RT), Wilhem Gidabuday alikiri kupata taarifa za kifo hicho na kusema waandaaji wa mbio ndio wenye kujua kila kitu.

Alisema mwanariadha huyo alikuwa wa ridhaa si wa kulipwa kama ilivyokuwa kwa wenzake.
Mwanariadha afa baada ya kuanguka ghafla kwenye mashindano ya Kili Marathon Mwanariadha afa baada ya kuanguka ghafla kwenye mashindano ya Kili Marathon Reviewed by Zero Degree on 2/27/2017 12:56:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.