Loading...

Nahodha wa klabu ya Bayern Munich, Lahm atangaza kustaafu soka

Mchezaji wa klabu ya Bayern Munich Philipp Lahm ambaye pia ni nahodha wa timu hiyo na alikuwa pia nahodha wa timu ya taifa ya Ujerumani walipotwaa Kombe la Dunia mwaka 2014, ametangaza atastaafu soka mwisho wa msimu huu.

Mchezaji huyo ambaye ana miaka 33 ametangaza uamuzi huo baada ya Bayern kushinda mechi ya hatua ya 16 bora katika michuano ya Kombe la Ujerumani dhidi ya Wolfsburg.

Ilikuwa mechi yake ya 501 kwake kuchezea viongozi hao wa Bundesliga.

“Ninaweza kuendelea na mtindo wangu wa uongozi, kujitolea kila siku, kila kipindi cha mazoezi, hadi mwisho wa msimu. Ninaweza kuendelea kufanya hayo msimu huu lakini si zaidi ya hapo,” amesema.

Hii ina maana kwamba ataondoka klabu hiyo mwaka mmoja kabla ya mkataba wake kumalizika.

Amesema amekuwa akitafakari kuhusu uamuzi huo kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Alicheza mechi yake ya kwanza katika kikosi cha wachezaji wakubwa Bayern mwaka 2002 na ameshinda mataji saba ya Bundesliga akiwa na klabu hiyo, pamoja na Kombe la Ligi ya Klab

Alitangaza kustaafu kutoka kwa timu ya taifa baada ya kushinda Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka 2014.
Nahodha wa klabu ya Bayern Munich, Lahm atangaza kustaafu soka Nahodha wa klabu ya Bayern Munich, Lahm atangaza kustaafu soka Reviewed by Zero Degree on 2/08/2017 12:49:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.