Loading...

Rais wa FIFA, Gianni Infantino aibeba tena Africa kwenye kombe la dunia

RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani (Fifa), Gianni Infantino, amesisitiza kwamba lazima Afrika iwe na wingi wa timu kwa maana ya uwakilishi mpana zaidi katika fainali za Kombe la Dunia kwa miaka ijayo.

Infantino ameviambia vyombo vya habari nchini Afrika Kusini kwamba dhamira yake ni kuhakikisha kwamba uwakilishi wa Afrika unakuwa mkubwa na mpana zaidi ya maeneo mengine duniani.

Infantino ameeleza kwamba Afrika ni bara kubwa ambalo linahitaji kuwa na uwakilishi mpana zaidi ikilinganishwa na maeneo mengine duniani.

“Afrika ni bara kubwa ambalo linahitaji uwakilishi bora na mpana pengine kuliko maeneo mengine duniani hasa tunapozungumzia suala la Kombe la Dunia,” alisema Infantino.
Rais wa FIFA, Gianni Infantino aibeba tena Africa kwenye kombe la dunia Rais wa FIFA, Gianni Infantino aibeba tena Africa kwenye kombe la dunia Reviewed by Zero Degree on 2/26/2017 04:57:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.