Loading...

Niyonzima awaomba radhi mashabiki wa Yanga

Kiungo na nahodha wa yanga, Haruna Niyonzima 
Baada ya kuzidiwa maarifa na wachezaji wa Simba, kiungo na nahodha wa yanga, Haruna Niyonzima amewaomba radhi mashabiki wa klabu hiyo kwa kupoteza mchezo dhidi ya Simba licha ya kuwa na nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi.

Niyonzima ambaye hulalamikiwa mara zote kwa kucheza chini ya kiwango hasa mpambano wa mahasimu, alisema jambo lililowagharimu ni kushindwa kutumia nafasi nyingi walizopata.

Nahodha huyo amesema mechi ilikuwa rahisi lakini walizembea kumaliza kazi mapema na kuwaruhusu Simba kupata nguvu ya kuwaadhibu.

"Sikufurahishwa na matokeo kwani tulikuwa na kila sababu ya kushinda mchezo huu, tena kuumaliza kipindi cha kwanza, lakini tulishindwa kutumia nafasi nyingi tulizopata na hilo ndilo lililotugharimu.

"Kama tungetumia vizuri nafasi tulizopata, mechi tulikuwa tunaimaliza kipindi cha kwanza, lakini sijui hata tulipatwa na nini tukapotea na wapinzani wetu wakatushinda," amesema Niyonzima.

Source: Mwananchi
Niyonzima awaomba radhi mashabiki wa Yanga Niyonzima awaomba radhi mashabiki wa Yanga Reviewed by Zero Degree on 2/26/2017 04:43:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.