TCRA yaeleza jinsi ya kuhama mtandao mmoja wa simu kwenda mwingine bila kubadili namba ya simu
Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano (TCRA) imezindua mpango wa elimu kwa umma kuhusu hudumu ya kuhama mtandao mmoja wa simu kwenda mwingine bila kubadili namba ya simu ya kiganjani (MNP).
Akizindua mpango huo leo Jumatano asubuhi, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amesema lengo ni kuwapa uhuru wateja kutumia mtandao bora zaidi, pia kuongeza ushindani kwa watoa huduma na kuboresha huduma zao.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba |
Kilaba amesema mabadiliko hayo ni mwendelezo wa maendeleo ya teknolojia nchini ukizingatia kwamba watumiaji wa simu wameongezeka kutoka milioni 2.9 mwaka 2005 mpaka kufikia milioni 40.1 Disemba, 2016.
"Uanzishwaji wa MNP ni kwa mujibu wa kanuni za mwaka 2011. Kanuni hizi zinawataka watoa huduma za simu za kiganjani kuwezesha huduma hii katika mitandao yao."
"Uanzishwaji wa MNP ni kwa mujibu wa kanuni za mwaka 2011. Kanuni hizi zinawataka watoa huduma za simu za kiganjani kuwezesha huduma hii katika mitandao yao."
TCRA yaeleza jinsi ya kuhama mtandao mmoja wa simu kwenda mwingine bila kubadili namba ya simu
Reviewed by Zero Degree
on
2/22/2017 03:17:00 PM
Rating: