Loading...

Watuhumiwa 19 mbaroni kwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya mkoani Iringa

VITA ya dawa za kulevya iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, imevuka mipaka na sasa imetua mkoani Iringa ambako watuhumiwa 19, wakiwamo wafanyabiashara na watumiaji wametiwa mbaroni.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Iringa, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, alisema mapambano hayo sasa yatakuwa endelevu kama njia ya kukomesha biashara hiyo.



“Pamoja na kuwakamata watuhumiwa ambao wanahusishwa na biashara hii, si wao tu, pia tumewakamata hata watumiaji ili kuweza kupata maelezo ya kina ni wapi wanaponunua na nani anawauzia.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Julius Mjengi, alisema Jeshi la Polisi litaendelea na msako mkali ili kuweza kuwatia mbaroni watu wanaofanya biashara hiyo na watumiaji.

Alisema kuwa kati ya watuhumiwa hao, 14 ni ‘mateja’ ambao wameathirika kwa utumiaji wa dawa za kulevya na watano ni wafanyabiashara wa dawa hizo haramu.
Watuhumiwa 19 mbaroni kwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya mkoani Iringa Watuhumiwa 19 mbaroni kwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya mkoani Iringa Reviewed by Zero Degree on 2/08/2017 12:32:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.