Loading...

Alichosema Cannavaro kuelekea mechi ya Yanga na Azam

ZIKIWA zimebaki siku mbili kabla ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Yanga na Azam, nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro', amesema mchezo huo ni muhimu zaidi kwao, hivyo wapinzani wao hao hawatatoka ‘salama’ uwanjani.

Cannavaro, alisema kuwa, wanataka kubaki kwenye mbio za ubingwa na wanafahamu kupoteza mchezo huo watakuwa wamejiweka katika wakati mgumu kutetea ubingwa wao.

Alisema anafahamu Azam nao wataingia kwa nia ya ushindi, lakini watapambana kwa ajili ya kutetea ubingwa wao.

"Najua mchezo utakuwa mgumu. Kumekuwa na mchezo mgumu kila tunapokutana, lakini ni lazima tupiganie ushindi ili kuendelea kuupigania ubingwa wetu," alisema Cannavaro.

Aidha, alisema kwa namna msimamo wa ligi ulivyo hawapaswi kuteleza kwenye michezo iliyobaki kwa kuwa kufanya hivyo ni kutoa nafasi kwa wapinzani kujihakikishia ubingwa.

Yanga inashika nafasi ya pili nyuma ya Simba ikiwa na pointi 53 ikiachwa kwa pointi mbili huku Azam ikifuata kwa pointi 44.
Alichosema Cannavaro kuelekea mechi ya Yanga na Azam Alichosema Cannavaro kuelekea mechi ya Yanga na Azam Reviewed by Zero Degree on 3/29/2017 11:47:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.