Loading...

Aliyekuwa Rais wa Korea Kusini, Park Geun-hye amekamatwa Ijumaa hii

Rais wa zamani wa Korea Kusini Park Geun-hye, aliyeondolewa madarakani mapema mwaka huu, amekamatwa Ijumaa hii.

Kwa mujibu wa jaji, kukamatwa kwa Bi. Park kumetokana na hofu kuwa anaweza kujaribu kuharibu ushahidi wa makosa anayotuhumiwa. Waendesha mashtaka walitangaza Jumatatu kuwa walikuwa wakifuatilia kukamatwa kwake kwa mashtaka yanayohusiana na kutumia vibaya madaraka, ufisadi na kuvujisha taarifa muhimu.

Park alikuwa ameshikiliwa kwa muda katika ofisi maalum za mwendesha mashtaka wa Seoul. Amepelekwa kwenye kituo cha kizuizi cha Seoul Ijumaa hii ambako mshirika wake Choi Soon-sil na watu wengine mashuhuri wanaohusishwa na mashtaka hayo akiwemo mrithi wa Samsung, Lee Jae-yong wanashikiliwa pia.

Park bado hajasomewa mashtaka rasmi. Aliondolewa madarakani March 10 baada ya mahakama ya kikatiba kuamua kumuondoa kutokana na madai ya ufisadi.
Aliyekuwa Rais wa Korea Kusini, Park Geun-hye amekamatwa Ijumaa hii Aliyekuwa Rais wa Korea Kusini, Park Geun-hye amekamatwa Ijumaa hii Reviewed by Zero Degree on 3/31/2017 10:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.