Loading...

Baada ya uchunguzi wa kina juu ya chanzo cha kifo cha msanii George Michael, hili ndilo lililobainika

Hatimaye uchunguzi uliokuwa ukiendelea kwa miezi sasa kuhusu kilichokuwa chanzo cha kifo cha nguli wa muziki wa Pop mwenye asili ya UK George Michael umekamilika.

Awali baada ya kuiaga dunia mwezi Disemba siku ya sikukuu za krismasi, hakuna aliyejua ni nini haswa ilikuwa sababu ya kifo chake, huku familia pia ikishindwa kutoa taarifa kamili kuhusu kilichotokea.

Baada ya tetesi nyingi kuzuka kutokana na kifo chake, wengi wakidai kwamba muimbaji huyo nguli alijitoa uhai, wengine pia wakikadiri kwamba huenda alifariki kwa sababu ya utumiaji wa dawa za kulevya, familia yake iliamuru kufanyika kwa ‘post-moterm’ ili kuweka kila kitu wazi.

Michael George alikutwa akiwa amefariki nyumbani kwake. Hadi kifo chake, alikuwa na umri wa miaka 53. Tarehe 7 siku ya Jumanne ndo siku ambayo madaktari walio na utaalam katika masuala hayo wamewasilisha ripoti rasmi iliyobeba matokeo ya uchunguzi waliofanya kuhusu kifo cha marehemu kwa familia. Uchunguzi huo uliendelea kwa muda wa karibia miezi mitatu. Imebainika George Michael alifariki kutokana na sababu za kawaida (natural causes) na sio vingine.

Ni ripoti ambayo bila shaka imewapa afueni mashabiki za mwanamuziki huyu aliyekuwa mkongwe.

Itakumbukwa kwamba George aliwahi kutuhumiwa kwa kashfa kibao pamoja na ya kushiriki katika utumiaji wa dawa za kulevya ambapo mwaka wa 2010 alifungwa kwa miezi miwili baada ya kusababisha ajali kwa kuendesha gari akiwa mlevi wa dawa za kulevya.

Licha ya hayo yote, alizidi kupokea love kutoka kwa mashabiki wa muziki wake na taarifa za kifo chake ziliwashtua wengi.
Baada ya uchunguzi wa kina juu ya chanzo cha kifo cha msanii George Michael, hili ndilo lililobainika Baada ya uchunguzi wa kina juu ya chanzo cha kifo cha msanii George Michael, hili ndilo lililobainika Reviewed by Zero Degree on 3/08/2017 10:26:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.