Loading...

BASATA yatoa Tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye masomo ya sanaa

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limetoa tuzo kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini waliofanya vizuri kitaifa katika masomo ya sanaa.

Wakati akizungumza kwenye sherehe ya utoaji tuzo hizo iliyofanyika katika ukumbi wa BASATA jijini Dar es Salaam, Mgeni rasmi ambaye ni Rais wa Shirikisho la Sanaa za Maonyesho Tanzania, William Chitanda ameitaka serikali kupitia baraza hilo kurudisha masomo ya sanaa kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu.

Amesema kuwa, serikali haina budi kuheshimu sanaa na wasanii kwa kuwa kazi zao huingizia kipato pamoja na kutoa ajira kwa vijana.

“Sanaa ni muhimu, badala ya serikali kuichukulia kama burudani sasa waione kama chanzo cha ajira na mapato yake kupitia kodi zinazotozwa kupitia kazi za wasanii,” amesema.

Amewataka wanafunzi kutodharau masomo ya sanaa, na kuwataka kusoma masomo hayo kwa kuwa huongeza hali ya ufaulu darasani.

Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza amesema lengo la baraza hilo kutoa tuzo ni kujenga hamasa, hari na ubunifu katika kuleta maendeleo kupitia masomo ya sanaa.

Baadhi ya wanafunzi waliopewa tuzo hizo ni Josia Soi na Shedrack Wilson kutoka shule ya sekondari Royola ambao walifanya vizuri katika somo la muziki.

Wengine ni Benjamin Kulwa aliyefaulu somo la uchoraji kutoka shule ya sekondari Azania, Amosi Kamgisha wa Sekondari ya Bukoba kupitia somo la Uchoraji, na Mary Mkonye kutoka shule ya sekondari Darajani aliyefaulu somo la sanaa ya maonyesho.
BASATA yatoa Tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye masomo ya sanaa BASATA yatoa Tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye masomo ya sanaa Reviewed by Zero Degree on 3/28/2017 12:30:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.