Loading...

FIFA yaidhinisha kuwepo kwa timu 48 kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 2026

Kuwepo kwa timu 48 ilikua ni moja ya ahadi ya Gianni Infantino katika kampeni zake
Chama cha soka duniani FIFA kimepanga kuwepo kwa mechi 6 ili zipatikane timu zitakazoingia katika fainali za kombe la dunia mwaka 2026.

FIFA imefafanua ni kwa namna gani timu 48 zitaweza kushiriki michuano hiyo.

Rais wa shirikisho la soka Ulaya Aleksander Ceferin amesema kuwa amefurahishwa na hatua hiyo na nchi za Ulaya zitawakilishwa vyema.
Mchakato huo utakuwaje?

Kila mwanachama wa FIFA atakuwa na uwezo wa kuongeza walau timu moja katika michuano ya mwaka 2026.



Ujerumani ndio bingwa mtetezi wa kombe la dunia.
Mwenyeji wa fainali hizi ataingia moja kwa moja kama ilivyokua awali. Na hadi hivi sasa, Ujerumani ndio bingwa mtetezi wa kombe la dunia.

Mapendekezo hayo yapo hivi:
  • Afrika - Timu 9 kutoka timu za 5 za awali
  • Asia - Timu 8 kutoka timu 4 za awali
  • Ulaya - 16 kutoka timu 13 za awali
  • Marekani ya Kaskazini, Kati na Caribbean - Timu 6 kutoka timu 4 za awali
  • Bara la Oceania - inabakia vile vile Timu 1 kama ilivyokuwa awali
  • Amerika ya Kaskazini - Timu 6 kutoka timu 4 za awali
Hatua ya nyongeza ya timu hizo inatajwa kama sababu mojawapo ya kuonekana kwa nchi ambazo zilikuwa hazipati nafasi ya kushiriki mashindano hayo.

Mwezi januari chama hicho chenye mamlaka makubwa ya soka duniani, kilipanga kuongeza timu zitakazoshiriki michuano ya kombe la dunia kutoka 32 mpaka 48 na hii itaanza mwaka 2026.
FIFA yaidhinisha kuwepo kwa timu 48 kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 2026 FIFA yaidhinisha kuwepo kwa timu 48 kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 2026 Reviewed by Zero Degree on 3/31/2017 03:27:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.