Loading...

Simba SC yawatoa hofu mashabiki kuhusu nyasi zinazodaiwa kodi Bandarini

Klabu ya Simba SC ambayo inadaiwa kodi na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya nyasi za bandia ilizoingiza nchini imewatoa hofu mashabiki wa klabu hiyo kufuatia kuwepo kwa taarifa kuwa nyasi hizo zitapigwa mnada.

Katika taarifa ya Simba ambayo imewekwa katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram imeelezea kuwa ni kweli wanadaiwa kodi lakini wanafanya jitihada za kulipa kodi hiyo.

Pia imewatoa hofu mashabiki huku ikiwataka waendelee kuishabikia timu yao kwa michezo iliyo mbele yao ya Ligi Kuu ya Vodacom ambapo kwa jumapili ya Aprili, 2 itapambana na Kagera Sugar.
Simba SC yawatoa hofu mashabiki kuhusu nyasi zinazodaiwa kodi Bandarini Simba SC yawatoa hofu mashabiki kuhusu nyasi zinazodaiwa kodi Bandarini Reviewed by Zero Degree on 3/31/2017 03:04:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.