Loading...

Hatimaye Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema aachiwa kwa dhamana

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema) Godbless Lema, ameachiwa kwa dhama leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Lema ameachiwa kwa dhamana ikiwa ni takribani miezi minne tangu awekwe rumande kwa kesi ya uchochezi.

Baadhi ya Wanachama wa CHADEMA wakishangilia kwa furaha baada ya Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema kuachiwa kwa dhamana mahakama kuu leo jijini Arusha. 
Polisi wa kutuliza ghasia walijaa mahakamani hapo wakiwafukuza wafuasi wa Lema waliojaa katika viwanja vya mahakama hiyo.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe walikuwepo mahakamani hapo leo.


Katika kesi hiyo iliyotolewa maamuzi majira ya saa 7:30 mchana, Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Mjini baada ya kupitia hoja za mawakili pande zote imemwachia kwa dhamana hiyo kwa masharti ya wadhamini wawili na kusaini bondi ya shilingi milioni tatu.

Lema amekaa mahabusu kwa takribani miezi minne sasa tangu alipokamatwa mwezi Novemba mjini Dodoma na kusafirishwa kupelekwa Arusha kisha kufunguliwa kesi ya uchochezi.
Hatimaye Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema aachiwa kwa dhamana Hatimaye Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema aachiwa kwa dhamana Reviewed by Zero Degree on 3/03/2017 03:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.