Loading...

Hatimaye Serikali ya Malaysia yakubali kuachia mwili wa ndugu wa Kiongozi wa Korea Kaskazini

Mwili wa Kim Jong-nam, aliyekuwa kaka wa kambo wa Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un umewasili mjini Pyonyang kutoka chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Kuala Lumpur nchini Malaysia baada ya Korea Kaskazini kutimiza sharti la kuwachia huru raia tisa wa Malaysia waliozuiliwa kuondoka nchini humo.

Nchi hizo mbili zimekuwa na mgogoro wa kidiplomasia kufuatia mauaji ya marehemu Kim Jong-nam yaliyotokea mwezi uliopita nchini Malaysia ambapo nchi zote mbili zilizuia raia wa nchi hizo kuondoka.

Raia hao tisa wa Malaysia waliwasili mapema leo,na kukutana na ndugu zao katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur pamoja na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Anifan Aman.

Miongoni mwa raia hao ni wafanyakazi wa ubalozi wa Malaysia nchini Korea Kaskazini na familia zao, na mshauri wa rais wan chi hiyo nchini Korea Kaskazini, Mohd Nor Azrin Md Zain.
Hatimaye Serikali ya Malaysia yakubali kuachia mwili wa ndugu wa Kiongozi wa Korea Kaskazini Hatimaye Serikali ya Malaysia yakubali kuachia mwili wa ndugu wa Kiongozi wa Korea Kaskazini Reviewed by Zero Degree on 3/31/2017 09:46:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.