Loading...

Conte azua gumzo baada ya kupeleka ombi hili mbele ya uongozi wa Klabu ya Chelsea

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vilivyotoa ripoti inayodai kwamba, Conte 'Aliuomba uongozi Chelsea kuchelewesha mazungumzo yote juu ya mikataba na wachezaji wake hadi pale wataposhinda Kombe la Ligi Kuu.'

Express Sport inaripoti kwamba, 'Real Madrid sasa wako tayari kulipa kiasi cha paundi milioni 100 kwa ajili ya kumsajili Edeni Hazard, ikiwa wataiona dalili yoyote yeye [Hazard] kutaka kujiunga na klabu hiyo.'

Thibaut Courtois na Diego Costa nao pia wanadaiwa kutaka kuondoka, Hata hivyo, kuna uwezekano mdogo sana kwa Chelsea kuwauza wachezaji wao wenye majina makubwa.

Lakini, vyombo vikuu vya habari vinaendelea kutoa taarifa ya muitaliano huyo kuitaka 'The Blues' kuzuia utoaji wa nafasi ya mazungumzo yoyote kwa yeye mwenyewe au wachezaji wake.

Vyanzo vingi vinadai kuwa tayari mikataba ya Conte na wachezaji hao watatu wa Chelsea [Hazard, Costa na Courtois] ilishaandaliwa mezani kwa wote kusaini, ambavyo zoezi hilo linatarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Conte azua gumzo baada ya kupeleka ombi hili mbele ya uongozi wa Klabu ya Chelsea Conte azua gumzo baada ya kupeleka ombi hili mbele ya uongozi wa Klabu ya Chelsea Reviewed by Zero Degree on 3/31/2017 11:24:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.