Loading...

Nani atamaliza katika 4 bora? Nani atakwama Ligi kuu ya Uingereza?

Ligi ya Uingereza inaelekea ukingoni,hakuna uhakika 100% kama Chelsea wanaweza kuwa mabingwa japo wanapewa nafasi kubwa, ukiwaacha Chelsea hebu tuone vita ya top four msimu huu.

Tottenham Hotspur. Wako nafasi ya pili msimu huu hadi sasa, lakini tofauti ya alama kati yao na Manchester United walioko nafasi ya 5 ni alama saba tu. 

Michezo ya Tottenham iliyosalia sio mirahisi kwao kwani wana michezo 6 ugenini dhidi ya West Ham, Leicester City,Burnley, Swansea, Crystal Palace na Hull City lakini mechi za nyumbani sio rahisi hata kidogo kwani ukiacha michezo dhidi ya Watford na Fc Bournamouth watakuwa na kibarua kigumu kuzikaribisha Manchester United na Arsenal ambao nao wanaitaka top four, wameshacheza michezo 28

Man City. City wako nafasi ya 3 ya msimamo wa ligi ya Uingereza wakiwa na alama 57, hii ni tofauti ya alama 5 tu na United ambao hawako top four huku timu hizi zikiwa bado hazijarudiana. 

City ana mechi ngumu wiki mbili zijazo na zote ni ugenini akiwafuata Arsenal na baadae Chelsea huku pia wakiisubiri United Etihad. Michezo mingine iliyobaki kwa Man City ni dhidi ya West Brom, Leicester, Middlesbrough, Crystal Palace, Watford, Hull City na Southampton, lakinini pia Man City nao wameshacheza michezo 28 kama Tottenham.

Liverpool. Liverpool ameshacheza michezo 29 ikiwa ni michezo miwili zaidi ya United, wamevuna alama 56 hadi sasa. Lakini labda pengine ni faida kwao kwani baada ya mchezo wao wa derby dhidi ya Everton, Liverpool wanaonekana watakuwa na michezo ya kwaida kwani hawatacheza na timu yoyote ambayo inawania top four kwa sasa, baada ya mchezo dhidi ya Everton wataikabili Bornamouth, Stoke City, West Brom, Crystal Palace, Watford, Southampton, West Ham na baadae Middlesbrough.

Manchester United. Walikaa nafasi ya 6 kwa siku zaidi ya 100 lakini sasa wako nafasi ya 5, tofauti yao na walioko juu yao ni kwamba wamecheza michezo michache zaidi kwani wamecheza michezo 27 huku wakiwa na alama 52. Lakini ugumi kwa Manchester United ni kwamba achilia mbali Everton lakini wana michezo migumu dhidi ya timu zingine zinazoitaka top four wana mchezo dhidi ya Chelsea,Man City,Arsenal na Tottenham. Huku pia wakicheza na West Brom, Sunderland, Burnley, Swansea, Crystal Palace na mwisho Southampton.

Arsenal. Kuanzia msimu wa 1995/1996 hawajawahi kumaliza ligi nje ya top four lakini msimu huu hilo linawanyemelea, wako nafasi ya 6 huku wakiwa na alama 50 lakini nao wakiwa wamecheza michezo 27. Katika mechi zao 11 zilizobaki Arsenal watakumbana na upinzani mkubwa toka kwa Man United,Man City na Tottenham, lakini pia watawakabili Everton ambao nao ni janga kwao huku pia wakicheza dhidi ya West Ham, Crystal Palace, Middlesbrough,Leicester City, Stoke, Sunderland na Southampton.
Nani atamaliza katika 4 bora? Nani atakwama Ligi kuu ya Uingereza? Nani atamaliza katika 4 bora? Nani atakwama Ligi kuu ya Uingereza? Reviewed by Zero Degree on 3/31/2017 11:32:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.