Hungary kujenga kiwanda cha kuunda mabasi nchini Tanzania
Balozi wa Hungary nchini, Lazaro Mathe amemweleza Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli kuwa serikali ya nchi yake ina mpango wa kujenga kiwanda cha kuunda mabasi nchini.
Mathe alimwambia Rais Magufuli mpango huo katika mazungumzo yaliyofanyika Ikulu ya Dar es Salaam muda mfupi baada ya balozi huyo kukabidhi hati za utambulisho.
Aidha Mathe alipongeza utendaji kazi wa Rais Magufuli na kuahidi serikali ya Hungary itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuendeleza sekta ya viwanda na tayari wawekezaji kutoka Hungary wameanza kufanya mchakato wa kujenga kiwanda cha kuunda mabasi ya abiria.
Zaidi waweza kusoma taarifa ya Kurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu kuhusu mazungumzo ya Mathe na Rais Magufuli.
Aidha Mathe alipongeza utendaji kazi wa Rais Magufuli na kuahidi serikali ya Hungary itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuendeleza sekta ya viwanda na tayari wawekezaji kutoka Hungary wameanza kufanya mchakato wa kujenga kiwanda cha kuunda mabasi ya abiria.
Zaidi waweza kusoma taarifa ya Kurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu kuhusu mazungumzo ya Mathe na Rais Magufuli.
Hungary kujenga kiwanda cha kuunda mabasi nchini Tanzania
Reviewed by Zero Degree
on
3/24/2017 11:00:00 AM
Rating: