Loading...

Jamhuri yakana kumshikilia Mfanyabiashara Yusuf Manji

SUALA la mfanyabiashara Yusuf Manji kuwa chini ya ulinzi kwa siku 28 katika Hospitali ya Agha Khan limechukua sura mpya baada ya Jamhuri kukana kwa kiapo kwamba haimshikilii mfanyabiashara huyo.

Hayo yalidaiwa jana katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam mbele ya Jaji Ama–Isario Munisi wakati maombi ya Manji ya kutaka aachiwe kizuizini kwa sababu anashikiliwa isivyo halali, yalipotaka kuanza kusikilizwa.

Mahakama Kuu ilipokea maombi kutoka kwa mawakili wa Manji, Hudson Ndusyepo, Alex Mgongolwa na Jeremiah Ntobesya wakidai mteja wao anashikiliwa isivyo halali, hivyo wanaiomba mahakama imwachie huru.

Lakini Wakili wa Serikali Mkuu, Osward Tibabyekomya, aliwasilisha majibu ya kiapo kinzani kuhusiana na maombi hayo.

Alidai aliwasilisha mahakamani majibu ya viapo viwili kinzani, kimoja kikiwa kimeapwa na Mpelelezi kutoka Idara ya Uhamiaji, Anord Munuo na cha pili kutoka ofisi ya Mwananasheria Mkuu wa Serikali, kilichoapwa na Salum Ndalama.

Wakili alidai katika viapo vyote viwili, waapaji wanasema Manji hashikiliwi na Polisi wala Uhamiaji.

Akijibu, Wakili Mgongolwa alidai Manji anashikiliwa na Uhamiaji na analindwa na polisi kwa siku 28 sasa.

Alisema walipofika kwa mara ya kwanza mahakamani walinzi hao walitumia gari lake kumfikisha mteja wake mahakamani.

“Mheshimiwa Jaji, hata leo Manji kaletwa chini ya ulinzi, askari wamemfikisha mahakamani wenyewe wakakaa nje.

“Mara ya kwanza walitumia gari langu…hata leo walitaka kutumia gari langu lakini wakaamua kumleta na gari lao.

“Mheshimiwa Jaji, Manji analindwa na polisi sita, tunaomba tupewe muda wa kujibu majibu ya kiapo kinzani na iwekwe kwenye kumbukumbu za mahakama kwamba hashikiliwi kama wanavyodai Jamhuri.

“Sisi hatuwezi kuwa wendawazimu tulete maombi mahakamani kuomba aachiwe kizuizini wakati hajashikiliwa,”alidai Mgongolwa.

Jaji Munisi alisema majibu ya kiapo kinzani yote mawili yanaeleza kwamba Yusuf Manji hajashikiliwa.

“Nashangaa, najiuliza maswali kwa nini Jamhuri wanasema hawajamshikilia? Waleta maombi wanasema anashikiliwa…!

Source: Mtanzania
Jamhuri yakana kumshikilia Mfanyabiashara Yusuf Manji Jamhuri yakana kumshikilia Mfanyabiashara Yusuf Manji Reviewed by Zero Degree on 3/21/2017 03:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.