Loading...

JTWZ inadaiwa Bilioni 3 na Shirika la Umeme nchini [Tanesco]

Mkuu wa Majeshi nchini, Evance Mabeyo amesema Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) linadaiwa Sh3 bilioni na Shirika la Umeme nchini na kesho (Jumatatu) watapunguza deni hilo ili wasikatiwe umeme.

Mkuu wa Majeshi nchini, Evance Mabeyo
Mabeyo ameyasema hayo leo wakati anazungumza na waandishi wa habari makao makuu ya jeshi (Ngome) na kueleza deni hilo limetokana na shughuli za jeshi hilo kwenye ulinzi wa Taifa pamoja na ufinyu wa bajeti. 

"Baada ya kupokea maelezo ya Tanesco na kufuatia tamko la Rais, Jeshi la Wananchi limetafakari na limefanya jitihada kupata fedha za kupunguza deni hili, tunadaiwa fedha kiasi kinachozi kidogo Sh3 bilioni, nimeagiza watendaji wetu watafute Sh1 bilioni," amesema Mabeyo.

Mabeyo amesema juhudi zinazofanywa na Jeshi hilo zinatakiwa kuonyeshwa na Taasisi nyingine ili kuweza kuiongezea Tanesco uwezo wa kutoa huduma.
JTWZ inadaiwa Bilioni 3 na Shirika la Umeme nchini [Tanesco] JTWZ inadaiwa Bilioni 3 na Shirika la Umeme nchini [Tanesco] Reviewed by Zero Degree on 3/26/2017 06:07:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.