Loading...

Kauli ya Kocha wa Burundi, Alain Oliver Niyungeko juu ya Mbwana Samatta

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Burundi Alain Oliver Niyungeko amesema anataka kukutana na Samatta kwa sababu itakuwa ni kipimo tosha kwa wachezaji wake na atakuwa akiangalia wachezaji wake watafanya nini baada ya kukutana na mshambuliaji huyo anaecheza soka la kulipwa kwenye klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji.

“Nimesikia habari za Samatta baada ya mechi dhidi ya Botswana nikasema huyo ndio namtaka ili niwaone wachezaji wangu wakimuona Samatta ambaye anacheza Ubelgiji watafanya nini. Ni vizuri kwetu kwa sababu mchezaji anapopata nafasi ya kucheza na mchezaji anayecheza nje anajituma ili kujipima nae.”

Kocha huyo amesema wachezaji wengi aliokuja nao ni wale anaowandaa kwa ajili ya michuano ya CHAN na hajaita wachezaji kutoka nje ya Afrika lakini akaonya kuwa, wasichukuliwe poa kwa sababu wanauwezo wa kutosha kupambana na Stars.

Amesema wachezaji wanaocheza nje ya Burundi ni Laudit Mavugo anayecheza Simba ya Tanzania pamoja na mchezaji mmoja anayecheza soka la kulipwa Msumbiji. Lengo la kutumia wachezaji wa ndani ni kuwandaa vyema kwa ajili ya mashindano ya CHAN ambayo yanahusisha wachezaji wanaocheza ligi za Afrika.
Kauli ya Kocha wa Burundi, Alain Oliver Niyungeko juu ya Mbwana Samatta Kauli ya Kocha wa Burundi, Alain Oliver Niyungeko juu ya Mbwana Samatta Reviewed by Zero Degree on 3/28/2017 02:31:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.