Loading...

Kiongozi wa upinzani Niger ahukumiwa kwenda jela mwaka mmoja kwa kuuza watoto wachanga

Kiongozi wa upinzani nchini Niger Hama Amadou amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kupatikana na hatia ya kujihusisha na biashara haramu ya kuuza watoto wachanga kwa matajiri waliokuwa wanahitaji watoto hao.

Kiongozi huyo ambaye alishika nafasi ya pili kwenye uchaguzi uliofanyika mwaka jana alikuwa anajihusisha na biashara ya kununua watoto kutoka nchi jirani ya Nigeria.

Wakati hukumu hiyo ikitolewa, Amadou na mawakili wake hawakuwepo mahakamani na kila mara alikuwa akikanusha tuhuma hizo na kuzielezea kuwa ni za kisiasa.
Kiongozi wa upinzani Niger ahukumiwa kwenda jela mwaka mmoja kwa kuuza watoto wachanga Kiongozi wa upinzani Niger ahukumiwa kwenda jela mwaka mmoja kwa kuuza watoto wachanga Reviewed by Zero Degree on 3/14/2017 10:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.