Loading...

Kwanini nyanya ni maarufu zaidi duniani?

Ikiwa ungeulizwa kutaja tunda bora zaidi duniani , labda nyanya haitakuwa akilini mwako. Lakini unalolihitaji kulifahamu ni kuwa nyanya huzalishwa kwa wingi zaidi duniani kuliko tunda lolote lile.

Baadhi ya watu hudai kuwa tunda la embe ndilo maarufu zaidi duniani kwa misingi kuwa linaliwa kwenye nchi nyingi zaidi kuliko tunda lolote lile.

Lakini ikiwa utapima umaarufu kwa uzalishaji kote duniani, embe liko nyuma ya tufaa na hata ndizi.

Kuna zaidi ya tani 100 za ndizi ambazo huzalishwa kila mwaka huku India ikiwa ndio mzalishaji mkuu.

Shereha za La Tomatina
La Tomatina ni sherehe ambazo huandaliwa kila mwaka kwenye mji mdogo wa uhispania wa Bunol.

Wakati wa sherehe hizo karibu watu 40,000 hurushiana nyanya.

Nyanya inaweza kuliwa bila kupikwa au kwa kupikwa. Huku tani 170 za nyanya zikizalishwa kila mwaka, nyanya imeipiku hata ndizi.

Wengi huchukulia nyanya kama mboga lakini ukweli ni kwamba nyaya na tunda kwa sababu ina mbegu hali ambayo huiweka katika familia ya tunda.

Kuna zaidi ya aina 20,000 ya nyanya duniani.
Kwanini nyanya ni maarufu zaidi duniani? Kwanini nyanya ni maarufu zaidi duniani? Reviewed by Zero Degree on 3/04/2017 12:23:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.