Loading...

Madiwani wapigwa marufuku kuvaa jeans kwenye vikao

Madiwani jijini Tanga waliokuwa wakivaa suruali aina ya jeans kwenye vikao vya baraza wanalazimika kuachana na nguo hizo baada ya Meya wa jiji hilo, Mustafa Mhina kupiga marufuku uvaaji wa mavazi hayo.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani jana, Mhina alisema viongozi hao hawaruhusiwi kuvaa suruali hizo na mavazi mengine ambayo hayana staha.

Madiwani wa Ilala wakiwa katika kikao
Mhina amewataka madiwani kuvaa majoho na kofia na kwamba ambao hawatafuata utaratibu huo watatolewa nje ya mkutano.

Akichangia hoja, Diwani wa Maweni, Joseph Collivas (CCM) aliwataka wajumbe wa Baraza la Madiwani kutoa kero za wananchi ili zipatiwe ufumbuzi.
Madiwani wapigwa marufuku kuvaa jeans kwenye vikao Madiwani wapigwa marufuku kuvaa jeans kwenye vikao Reviewed by Zero Degree on 3/01/2017 09:31:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.