Loading...

Marekani yachoshwa na mienendo ya Korea Kaskazini

Sera ya Marekani ya kuwa na subira dhidi ya Korea Kaskazini imeisha, kulingana waziri wa maswala ya nje nchini humo Rex Tillerson wakati wa ziara yake nchini Korea Kusini.

''Njia zote tulizotumia ziko wazi na sasa tunatafuta njia nyengine za kidiplomasia , usalama na kiuchumi'' ,alisema.
Korea Kaskazini imezua wasiwasi kufuatia hatua yake ya hivi karibuni kufanyia majaribio makombora na silha za kinyuklia.

Bwana Tillerson alizungumza muda mfupi baada ya kuzuru eneo lisilo na wanajeshi linalozigawanya nchi hizo mbili za Korea.

Amesema kuwa juhudi za miaka 20 za kuibembeleza Korea Kaskazini kuachana na mipango yake ya kinyuklia zimegonga mwamba.

Alipoulizwa iwapo kuna uwezekano wa kuichukulia hatua za kijeshi alisema: Hatutaki kuchukua hatua kama hizo lakini akaongezea kuwa iwapo wataendeleza vitisho vyao hadi kufikia kiwango ambacho kinahitaji kuchukuliwa hatua basi hakutakuwa na chaguo jingine
Marekani yachoshwa na mienendo ya Korea Kaskazini Marekani yachoshwa na mienendo ya Korea Kaskazini Reviewed by Zero Degree on 3/18/2017 09:55:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.