Loading...

Mayweather ajibatiza jina jipya

BINGWA asiyepigika mwenye maneno mengi, Floyd Mayweather Jr, aliyecheza mapambano 49 na kushinda yote, ameamua kubadili jina na kuanza kujiita TBE (The Best Ever), yaani mkali wa milele.

Mkali huyo alisema ataanza kulitumia jina hilo kuanzia sasa, kauli ambayo aliitoa alipokuwa katika ziara ya kitalii nchini Uingereza.

“Pindi unapozungumzia mabondia wakongwe unataja mabondia bora waliocheza michezo zaidi ya 100, lakini ukiangalia rekodi mimi nimewapiga mabondia bora zaidi katika historia ya ngumi,” anasema.

Mayweather, mwenye umri wa miaka 40, alistaafu kucheza masumbwi mara baada ya kumtwanga Andre Berto katika pambano lililopigwa mwaka jana na kuhitimisha safari yake katika mchezo wa masumbwi kwa kushinda mapambano 49, huku 26 yakiwa kwa KO.

Bingwa huyo ameamua kurudi ulingoni kuzipiga na mkali wa ngumi mchanganyiko, Connor McGregor, ambaye mara kwa mara amekuwa akitamba kuvunja rekodi ya mkali huyo ya kutopoteza pambano.
Mayweather ajibatiza jina jipya Mayweather ajibatiza jina jipya Reviewed by Zero Degree on 3/12/2017 03:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.