Loading...

Nani kuwa Rais mpya wa Shirikisho la soka barani Afrika [CAF]?

Uchaguzi wa chama cha soka CAF unaenda kufanyika baada ya masaa kadhaa yajayo. Wagombea wawili ambao ni raisi wa sasa Issa Hayatou na raisi wa chama cha soka cha Madagascar Chief Ahmad wanaelekea kuwa na upinzani mkubwa katika nafasi hiyo ya uraisi wa CAF.

Tayari ripoti zinasema Ahmad ana dalili kubwa kumbwaga Hayatou katika uchaguzi huo utakaofanyika nchini Addis Ababa.Jarida moja la michezo nchini Nigeria linasema viongozi wa soka wa ukanda wa kusini (COSAFA) wamepanga kumpigia kura bwana Ahmad badala ya Hayatou.

Kiongozi mmoja wa soka kutoka ukanda huo amedai ana uhakika Ahmad atapatakura 14 ambazo ni sawa na 40% kutoka ukanda wao. COSAFA wanamtaka Ahmad kwa kuwa anatokea ukanda wao na wanaamini kumuweka yeye itakuwa na faida kwao kisoka.Lakini wakati huo huo imefahamika Ahmad ana uhakika 100% kupata kura kutoka Morocco,Egypt na baadhi ya kura kutoka CECAFA.

Wakati huo huo ripoti kutoka Nigeria zinasema serikali ya nchi hiyo imekiambia chama cha soka cha nchi hiyo kumpigia kura Hayatou. Makamu wa raisi wa nchi hiyo Yemi Osibanjo amemuambia raisi wa chama cha soka cha Nigeria (NFF) Ammaju Pinnick kumpigia kura Hayatou.

Suala la Nigeria kumpa sapoti Hayatou ambae ni Mcameroon si tu kwamba linatoka na ujirani kati ya Nigeria na Cameroon. Cameroon wamekuwa wakiisaidia Nigeria kupambana na kundi la magaidi la Bhoko Haram na hii inaonesha ni jinsi gani nchi hizi zinasaidiana na ndio maana serikali inaona bora kuendeleza ushirikaono huu katika uchaguzi wa CAF
Nani kuwa Rais mpya wa Shirikisho la soka barani Afrika [CAF]? Nani kuwa Rais mpya wa Shirikisho la soka barani Afrika [CAF]? Reviewed by Zero Degree on 3/15/2017 01:17:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.