Loading...

Nape Nnauye aikana akaunti feki ya twitter

Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, ameukanusha ujumbe unaotumwa kupitia akaunti ‘feki’ ya twitter yenye jina lake na kuwataka wanaofanya hivyo waache kwani anawafahamu na atawataja.

Nape ameandika hayo leo saa sita mchana baada ya akaunti hiyo feki kuandika:


“Amemzuia Kinana kuzungumza, akae akijua hakuna marefu yasiyokuwa na ncha”

Akaunti hiyo feki pia iliandika:

“Siyo wote wenye nidhamu ya woga kunyamazia udhalimu unaowafanyia, utawazuia watu kuzungumza hadi lini? Katibu wangu piga moyo konde”

Nape alikanusha na kuandika:

“Mnahangaika nini kunichafua kwenye twitter, hizi tweet zinazosambwa za maneno yasiyo na busara siyo zangu, nilishasema jana nikamaliza, nitawataja sasa!”

Leo asubuhi Nape aliandika ujumbe wa kuwashukuru wanahabari na kusema alikuwa hajui kama wanampenda kiasi kile.
Nape Nnauye aikana akaunti feki ya twitter Nape Nnauye aikana akaunti feki ya twitter Reviewed by Zero Degree on 3/24/2017 06:46:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.