Loading...

Okwi anavyozidi kuwatia kiwewe Simba SC

Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Emanuel Okwi, amezidi kuitia kiwewe klabu hiyo kutokana na kuendelea kung’ara nchini Uganda akiwa na kikosi cha SC Villa.

Okwi ambaye alivunja mkataba wake na kikosi cha Sonderjyske ya Denmark baada ya kuchoshwa na benchi, ameudhihirishia umma kuwa hajachoka kufuatia kucheka na nyavu.

Straika huyo mpaka sasa amecheka na nyavu mara sita ikiwemo ‘hat-trick’ katika mchezo wa Ligi Kuu Uganda dhidi nya Onduparaka, jambo linalowachanganya Wekundu wa Msimbazi ambao wamekuwa wakimmezea sana mate.

Mambo yamezidi kuwa mazuri kwa mshambuliaji huyo ambaye aliwahi kuichezea Yanga, ambapo atakuwa nahodha wa kikosi cha timu ya Taifa ya ‘Uganda Cranes’ kitakachocheza mechi ya kirafiki Machi 19, mwaka huu dhidi ya Eastern Region Select, mchezo huo umepangwa kufanyika kwenye Uwanja wa Kamuli Town.

Kocha wa msaidizi wa Uganda Cranes, Moses Basena ambaye aliwahi kumfundisha Okwi akiwa Simba, alimjumuisha mchezaji huyo katika orodha ya nyota 23 aliowataja wikiendi hii.

Source: Bingwa
Okwi anavyozidi kuwatia kiwewe Simba SC Okwi anavyozidi kuwatia kiwewe Simba SC Reviewed by Zero Degree on 3/17/2017 01:39:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.