Rais Magufuli achangia milioni 15 kumalizia jengo la Zahanati.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jjohn Pombe Magufuli amechangia shilingi Milioni kumi na tano kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa jengo la Zahanati ya Mnolela Jengo ambalo limejengwa kwa nguvu za wananchi kwa kiasi cha shilingi milioni 40.
Rais Magufuli akiwa njiani kuelekea mkoani Mtwara alisimama kata ya Mnolela kuzungumza na wananchi huku mbunge wa jimbo hilo Nape Nnauye aliposimama na kumuomba Rais kuwasaidia fedha kwa ajili ya umaliziaji wa jengo hilo kwani baadhi ya kinamama kujifungulia nje kutokana na uhaba wa vyumba.
Baada ya kupewa taarifa hiyo Rais Magufuli alishuka kwenye gari na kwenda kukagua jengo hilo ndipo alipozungumza na kusema yeye atachangia milioni kumi na tano huku halmashauri ya wilaya ya Lindi ichangie milioni 30 na mbunge wa jimbo la mtama achangie shilingi milioni kumi huku akiwashukuru wananchi kwa hatua hiyo.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa mnolela wakamshukuru Rais kwa kuchangia fedha kwa ajili ya kumalizia ujenzi huo.
Hata hivyo Rais Magufuli alilazimika kusimama tena kata ya madangwa kuzungumza na wananchi na katoa agizo kwa mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey zambi, kuwashughulikia viongozi wa ushirikia waliowadhulumu wakulima.
Source: ITV
Rais Magufuli achangia milioni 15 kumalizia jengo la Zahanati.
Reviewed by Zero Degree
on
3/05/2017 12:30:00 PM
Rating: