Loading...

Shehena nyingine ya viroba yakamatwa na jeshi la polisi mkoani Sigida.

Jeshi la Polisi mkoani Singida lina washikilia wafanya biashara wa wili wanao uza vinywaji vikali kwa kukutwa na shehena kubwa ya pombe ambazo zimepigwa marufuku na serekali aina ya viroba na zilizo fungaishwa katika Paketi za nailoni zaidi ya katoni 2600.

Kaimu kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Singida Mrakibu Mwandamizi wa jeshi la Polisi Isaya Mbungi, amesema wamefanikiwa kupata shehena hiyo baada ya kufanya upekuzi katika maghala ya wafanya biashara hao na kukuta mlundikano wa katuni za pombe za viroba.

Katika zoezi hilo jeshi la polisi liliambatana na kaimu afisa bishara wa manispaa ya Singida Bwana.Erick Sinkwembe , naye amesema katoni hizo zaidi ya elfumbili miasita zina thamani ya zaidi ya shilingi milioni miambili na kuwataka wenye pombe za viroba kusalimisha polisi kwani zoezi hilo lita kuwa endelevu sehemu zote zinazo uza vinywaji vikali.

Kwa upande wao wafanya biashara hao wamesema vinywaji hivyo walinunua tokea mwaka jana, wameiomba serekali kuwaongezea muda ili waweze kumaliza akiba hiyo, kwani wengine fedha walizo nunulia awali walikuwa wamekopa katika benki.

Source: ITV
Shehena nyingine ya viroba yakamatwa na jeshi la polisi mkoani Sigida. Shehena nyingine ya viroba yakamatwa na jeshi la polisi mkoani Sigida. Reviewed by Zero Degree on 3/11/2017 06:16:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.