Loading...

Stars yatoka kifua mbele kwa ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Burundi Taifa

Mshambuliaji Mbaraka Abeid Yusuf ameweka rekodi yake kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Burundi uliomalizika kwa Taifa Stars kuibuka na ushindi wa magoli 2-1.

Mbaraka ameitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha Stars, mchezo wa leo dhidi ya Burundi ulikuwa wa kwanza kwake na amefunga goli lake la kwanza kwenye timu ya taifa.

Goli lake lilikuja baada ya mabeki wa Burundi kujichanganya na kuruhusu Mbaraka kuuwahi mpira kisha kutandika shuti lililo mpita golikipa wa Nahimana Jonathani kisha kugonga post na kurudi tena uwanjani Mbaraka akamalizia kwa ulaini likiwa ni goli la pili kwa Stars kwenye mechi ya leo.

Kocha Salum Mayanga alimjumuisha Mbaraka Yusuf kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha Stars alichokitangaza March 13, 2017 baada ya mshambuliaji huyo kufanya vizuri kwenye klabu yake ya Kagera Sugar.

Mbaraka ana magoli nane kwenye ligi kuu Tanzania bara magoli manne nyuma ya kinara wa ufungaji Msuva mwenye magoli 12 hadi sasa.

Goli la kwanza limefungwa na Simon Msuva dakika ya 22 kipindi cha kwanza akiunganisha krosi iliyopigwa na Mohamed Hussein kisha kuongezewa kwa kichwa na Ajib ndipo Msuva akaachia mkwaju wa maana na kufunga goli la kwanza.

Ushindi wa Stars wa magoli 2-1 dhidi ya Burundi ni wa pili mfululizo tangu timu iwe chini ya Mayanga ambaye ameipokea kutoka kwa Charles Mkwasa. Ushindi wa kwanza ulikuwa ni wa magoli 2-0 dhidi ya Botswana Jumamosi ya juma lililopita.
Stars yatoka kifua mbele kwa ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Burundi Taifa Stars yatoka kifua mbele kwa ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Burundi Taifa Reviewed by Zero Degree on 3/28/2017 08:03:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.