Loading...

Canada kuihalalisha bangi ifikapo mwaka 2018

Canada kuhalalisha bangi ifikapo mwaka ujao
Matumizi ya bangi kwa kujiburudisha yatahalalishwa nchini Canada ifikapo tarehe mosi Julai mwaka 2018.

Serikali ya Canada itawasilisha mswada wa kuhalalisha bangi ifikapo Aprili kwa mujibu wa shirika la habari la serikali la CBC.

Taarifa ziliiambia CBC kuwa wanachama wa chama tawala cha Liberal hivi majuzi walijulishwa kuhusu mswada huo.

CBC imesema kuwa sheria hizo mpya zitaambatana na mapendekezo yaliyotolewa na jopo lililoteuliwa na serikali.

Baadhi ya mapendekezo hayo ni kuwa Canada itaruhusu kuuzwa kwa bangi kwa lengo la watu walio na umri wa zaidi ya miaka 18 
kujiburudisha.


Jopo kazi hilo pia lilipendekeza kuwa watu wazima wataruhusiwa kupanda hadi mimea minne ya bangi na wamiliki hadi gramu 30 ya bangi iliyokaushwa.

Kwa mujibu wa CBS, serikali itasimamia kusambazwa wa bangi na kuwapa leseni wazalishaji.

Ahadi wa waziri mkuu Justin Trudeau, ya kuhalalisha bangi imechochea uvumi katika sekta hiyo.

Wazalishaji kama makampuni ya Aphria, OrganiGram Holdings, na Canopy Growth, ambao ni wazalishaji wakubwa zaidi wa bangi ya kutibu, yamekuwa vipnzi kwa wawekezaji wa hisa.
Canada kuihalalisha bangi ifikapo mwaka 2018 Canada kuihalalisha bangi ifikapo mwaka 2018 Reviewed by Zero Degree on 3/28/2017 03:33:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.