Loading...

Mkazi wa wilayani Mbozi afariki baada ya kupigwa na radi

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Edward Mwenda (63) amekufa baada ya kupigwa na radi, kutokana na mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na radi kunyesha huku ikiacha uharibifu mkubwa wa mazao yanayotegemewa kwa chakula na biashara katika kijiji cha Ndolezi kata ya Mlangali wilayani Mbozi mkoani Songwe.

Familia ya ukoo wa Mwenda imeeleza kuwa kifo cha marehemu kimetokana na kupigwa na radi kufuatia mvua iliyonyesha tarehe 26 march mwaka huu jambo liliowaacha na masikitiko makubwa kwani marehemu Edward Mwenda wakati wa uhai wake alikuwa akitegemewa na ndugu pamoja na jamii kwa ujumla.

Wakati mvua hizo zikisababisha msiba kwa wakazi wa Mlangali, tayari zimeshaacha athari kubwa kwenye mazao mbalimbali ikiwemo mahindi, kahawa, migomba, karanga na alizeti huku wananchi wakitoa wito kwa wakulima ambao mazao yao yamesalimika kuyatumia kwa uangalifu kwani huenda yakasaidia kukabiliana na hali ngumu mwakani.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Mbozi Erick Ambakisye ametoa rai kwa wakazi wa vijiji vya jirani kuepuka kuuza mazao watakayovuna ili kunusuru hatari ya kukosekana kwa chakula huku afisa mtendaji wa kata ya Mlangali akibainisha hatua zilizohukuliwa na serikali kufuatia janga hilo ambapo ameeleza kuwa tayari waathirika wameanza kuorodheshwa ili majina yao yawasilishwe kwenye kamati ya maafa ya wilaya itakayotathmini namna ya kutoa msada.

Mkazi wa wilayani Mbozi afariki baada ya kupigwa na radi Mkazi wa wilayani Mbozi afariki baada ya kupigwa na radi Reviewed by Zero Degree on 3/28/2017 03:25:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.