Loading...

Taasisi ya Taaluma za Kiswahili [TATAKI] yalaani wasomi wanaokwamisha matumizi ya Kiswahili

Tataki imelaani vitendo vya wasomi, Profesa, na wataalamu mbalimbali wanaopinga matumizi ya lugha ya kiswahili katika nyanja mbalimbali ikiwamo kutumika kama lugha ya kufundishia.

Hayo yamesemwa leo (jumamosi), na Mkurugenzi wa Tataki, Ernesta Mosha wakati wa maonyesho ya wiki ya utafiti wa lugha ya kiswahili katika miradi mbalimbali iliyoandaliwa na taasisi hiyo kwa lengo la kukuza kiswahili.

Miradi hiyo ikiwamo ya kufundisha lugha ya kiswahili kwa wageni wanaoingia nchini kwa ajili ya kuwapatia Taaluma na namna ya kuwasiliana kwa kutumia lugha ya kiswahili.

Mosha alisema katika wiki hiyo ya utafiti iliyobeba kauli mbiu ya "utafiti wa uchumi wa viwanda na maendeleo ya kati " imelenga kuhamasisha wawekezaji kutoka nje kutumia lugha ya Kiswahili katika mawasiliano.

"Hakuna maendeleo ya viwanda kama hakuna mawasiliano wakati wa uzalishaji hivyo ni muhimu kutumia kiswahili ambacho ndio lugha inayoeleweka nchini" alisema.
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili [TATAKI] yalaani wasomi wanaokwamisha matumizi ya Kiswahili Taasisi ya Taaluma za Kiswahili [TATAKI] yalaani wasomi wanaokwamisha matumizi ya Kiswahili Reviewed by Zero Degree on 3/26/2017 12:08:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.