Loading...

Umesikia alichosema Kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps kuhusu Ng'olo Kante?

Kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps amesema kiungo wa Chelsea, N’Golo Kante ni miongoni mwa wachezaji bora duniani.

Tangu alipoifanikishia timu yake ya awali, Leicester City kutwaa taji la Ligi Kuu England, mchezaji huyo amekuwa na mafanikio katika soka akiwa chini ya kocha, Antonio Conte.


Kante mwenye miaka 25, kiwango chake kimemvutia kocha Deschamps ambaye anainoa Ufaransa kujiandaa na mechi za kufuzu Kombe la Dunia kabla ya timu yake kukutana kwenye mechi ya kirafiki ya Hispania.

“Amekuwa na sisi kwa muda mfupi. Hakucheza mechi zote. Hii inategemea na mfumo ambao ninauchagua,” alisema Deschamps alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. 

“Kiwango cha N’Golo kimeturidhisha. Alikuwa na Leicester City na sasa anafanya vyema akiwa na Chelsea msimu huu. Natumaini ana nafasi ya kutwaa taji jingine akiwa hapa England.”
Umesikia alichosema Kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps kuhusu Ng'olo Kante? Umesikia alichosema Kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps kuhusu Ng'olo Kante? Reviewed by Zero Degree on 3/21/2017 06:21:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.