Loading...

Utafiti: Sumu ya Bui bui ni tiba ya ugonjwa wa Kiharusi

WATAFITI kutoka Chuo Kikuu cha Queensland and Monash, walisafiri hadi kisiwa cha Fraser, Australia kuwawinda na kuwashika buibui hatari wa nchi hiyo.

Watafiti hao wanasema kuwa protini iliyopo katika sumu ya buibui inaweza kusaidia kulinda ubongo kutokana na jeraha baada ya kiharusi.

Inaelezwa kuwa wanasanyasi waligundua kwamba tiba ya protini hiyo ilifanya kazi ilipotumiwa katika panya wa maabara.

Wanasema ilionyesha kwamba inaweza kuwa tiba nzuri katika siku zijazo lakini haijajaribiwa kwa binadamu.
Utafiti: Sumu ya Bui bui ni tiba ya ugonjwa wa Kiharusi Utafiti: Sumu ya Bui bui ni tiba ya ugonjwa wa Kiharusi Reviewed by Zero Degree on 3/22/2017 01:03:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.