Loading...

VIDEO: Aliyekuwa Katibu Mkuu wa ACT jijini Dar, Mohamed Ngulangwa atimkia CUF

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam,Mohamed Ngulangwa ameachana na chama hicho na kujiunga na Chama cha Wananchi(CUF).

Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama,Prof.Ibrahim Lipumba amemkaribisha Ngulangwa rasmi leo mbele ya wajumbe wa baraza kuu la Uongozi leo Makao Makuu ya Chama hicho. 

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho,Ngulangwa amesema ameamua kukihama ACT baada ya kuona kuna ukakasi ndani yake.

"ACT ni chama cha Upinzani na chenye watu makini lakini sera zao na mipango inakwamishwa na watu ambao wao wanawaamini,"alisema.

Pamoja na mambo mengine,kikao hicho kimelenga kujadili ajenda 11 ikiwamo kuthibitisha majina ya Wakurugenzi waliochaguliwa na Mwenyekiti huyo wiki iliyopita.



Source: Mwananchi
VIDEO: Aliyekuwa Katibu Mkuu wa ACT jijini Dar, Mohamed Ngulangwa atimkia CUF VIDEO: Aliyekuwa Katibu Mkuu wa ACT jijini Dar, Mohamed Ngulangwa atimkia CUF Reviewed by Zero Degree on 3/25/2017 11:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.