Loading...

VIDEO: Maajabu ya soka, ..Barca yatinga robo fainali baada ya kuisambaratisha PSG kwa kichapo cha goli 6-1

Barcelona wamegeuza matokeo na kutinga robo fainali kwa kuizaba Paris Saint Germain kwa mabao 6-1 katika mchezo wa marudiano wa Klabu Bingwa Ulaya.

PSG waliingia kwenye mchezo huo wakiwa na goli 4 mkononi ambazo walishinda katika mechi iliyopita.

Sergi Roberto alifunga bao la 6 kwa mkwaju wa mwisho wa mchezo, na hivyo kufanya matokeo ya jumla kuwa 6-5 kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la Nou Camp.

Barcelona walifunga magoli matatu katika dakika saba za mwisho. Walikuwa wakiongoza kwa 3-1.
Wiki tatu zilizopita PSG iliifunga Barcelona magoli 4-0 mjini Paris.

Hatua ya kurejesha magoli yote hayo ni kubwa kuwahi kushuhudiwa katika historia ya UEFA, na sasa Barcelona wana kila nafasi ya kunyanyua kombe la Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka mitatu.

Katika mchezo mwingine, Pierre Emerick Aubameyang alipachika ‘hat trick’ na kuipeleka Borussia Dortmund katika robo fainali dhidi ya Benfica.

Aubameyang alifunga magoli matatu

Borussia Dortmund wameshinda kwa jumla ya magoli 4-1 katika mechi mbili walizocheza.


VIDEO: Maajabu ya soka, ..Barca yatinga robo fainali baada ya kuisambaratisha PSG kwa kichapo cha goli 6-1 VIDEO: Maajabu ya soka, ..Barca yatinga robo fainali baada ya kuisambaratisha PSG kwa kichapo cha goli 6-1 Reviewed by Zero Degree on 3/09/2017 12:59:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.