Loading...

Freeman Mbowe akumbana na kigingi kingine mahakamani

Baada ya Serikali kumwekea pingamizi mahakamani Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe katika maombi yake ili asikamatwe na hatimaye yakatupwa, imemwekea kigingi kingine kwenye kesi ya msingi.

Mbowe amefungua kesi ya kikatiba Mahakama Kuu dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Katika kesi ya msingi namba 1 ya mwaka 2017, Mbowe pamoja na mambo mengine anapinga mamlaka ya mkuu wa mkoa kukamata na kile anachokiita kudhalilisha watu.

Hivyo, anaiomba mahakama hiyo pamoja na mambo mengine itamke kuwa vifungu namba 5 na 7 vya Sheria ya Tawala za Mikoa vinavyowapa mamlaka wakuu wa mikoa na wilaya kuwakamata watu na kuwatia mbaroni viko kinyume cha Katiba.

Kesi hiyo inayosikilizwa na jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu likiongozwa na Sekieti Kihiyo akisaidiana na Pellagia Kaday na Lugano Mwandambo, ilitajwa jana na upande wa Serikali ukawasilisha pingamizi la awali, ukiiomba mahakama iitupilie mbali.

Kutokana na pingamizi hilo, pande zote walikubaliana kusikiliza pingamizi hilo kwa njia ya maandishi, mahakama ikaamuru upande wa Serikali uwasilishe mahakamani hapo hoja za pingamizi Machi 17.

Source: Mwananchi
Freeman Mbowe akumbana na kigingi kingine mahakamani Freeman Mbowe akumbana na kigingi kingine mahakamani Reviewed by Zero Degree on 3/09/2017 01:02:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.