Loading...

VIDEO: Ndege ya Shirika la Ndege la Peru iIliyokuwa na abiria 141 yateketea kwa Moto

Ndege moja ya shirika la ndege la Peru, Peruvian Airlines, iliyokuwa imewabeba abiria 141, imeshika moto baada ya kutua kwa dharura katika Uwanja wa Ndege wa Jauja, katika Milima ya Andes.

Ndege hiyo aina ya Boeing 737-300 ilikuwa ikitokea Lima, imeshika moto ikiwa katika Mji wa Andean uliopo katikati ya nchi ya Peru umbali wa kilomita 265 kutoka Lima (ilipoanzia safari yake).





Shirika hilo la ndege limesema wote waliokuwa ndani wameokolewa salama na hakuna aliyepata majeraha huku sababu ya moto huo ikitajwa kuwa ndege hiyo iliteleza na kutoka nje ya njia inayotumiwa na ndege kupaa na kutua.

Wazima moto walifanikiwa kuuzima moto huo wakati huo im,earifiwa kuwa uchunguzi umeanzishwa kuhusu kisa hicho.

VIDEO: Ndege ya Shirika la Ndege la Peru iIliyokuwa na abiria 141 yateketea kwa Moto VIDEO: Ndege ya Shirika la Ndege la Peru iIliyokuwa na abiria 141 yateketea kwa Moto Reviewed by Zero Degree on 3/29/2017 12:41:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.