Loading...

Viroba vyenye thamani ya zaidi ya bilioni 10 vyakamatwa Jijini Dar

Operesheni ya siku tatu ya kukamata pombe aina ya viroba imebaini mambo kadhaa ikiwemo baadhi ya vifungashio kutumika zaidi ya mara moja huku viroba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 10 vikikamatwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mkemia mkuu wa serikali Prof Samueli Manyele amesema sampuli zilizopimwa ubora wake ulijitosheleza isipokuwa uiano wa ujazo ulikuwa tatizo.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya chakula na dawa TFDA, Bw Hiiti Sillo mbali na kuelezea madhara waliyokuwa wanayapata watumiaji amepongeza hatua serikali iliyochukuwa na kuongeza kuwa itasaidia kwa kiasi kikubwa kuokoa nguvu kazi ya taifa.

Aidha serikali imesema viroba hivyo vimehifadhiwa hadi pale itakapotoa taarifa nyingine na wale ambao walikutwa na makosa mbalimbali ikiwemo kutokulipa kodi,kukosa vyeti vya kimazingira hasa wenye viwanda watafikishwa mahakamani, ambapo agizo la kupiga marufuku utengenezaji na utumiaji wa viroba ulitolewa na waziri mkuu Mh Kassim Majaliwa.
Viroba vyenye thamani ya zaidi ya bilioni 10 vyakamatwa Jijini Dar Viroba vyenye thamani ya zaidi ya bilioni 10 vyakamatwa Jijini Dar Reviewed by Zero Degree on 3/05/2017 08:28:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.