Wajawazito wanne wachangia kitanda kimoja katika Hospitali ya wilaya.
Hospitali ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma inakabiliwa na upungufu wa majengo na vitanda kwenye wodi ya wajawazito ambapo wajawazito wanalala wagonjwa wanne katika kitanda kimoja.
Hayo yamebainika katika kipindi hiki ambacho wanawake wako katika heka heka ya siku ya mwanamke duniani Machi 8 ambapo Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Mbinga Dkt Jordan Nchimbi amesema wodi ya wazazi ya hospitali hiyo ni ndogo kiasi ambacho hawawezi kuongeza vitanda na hivyo wajawazito wanalala wanne katika kitanda kimoja.
Wanawake watumishi katika Halmashauri ya mji wa Mbinga wametembelea wodi ya wajawazito katika hospitali hiyo kuona changamoto zinazowakabili wanawake na kutoa misaada mbalimbali ikiwemo mashuka ambapo pia wametoa misaada katika vituo vya watoto yatima.
Mganga huyo wa hospitali hiyo ya wilaya amewashukuru wanawake hao kwa misaada hiyo na kwamba mashuka hayo yatawasaidia wagonjwa katika wodi hiyo.
Source: ITV
Wajawazito wanne wachangia kitanda kimoja katika Hospitali ya wilaya.
Reviewed by Zero Degree
on
3/07/2017 12:43:00 PM
Rating: